Finland yasaini mkataba wa Sh3.9 bilioni na kampuni za misitu

Ubalozi wa Finland nchini umesaini mkataba wa makubaliano wa jumla ya Euro 1.6 milioni (bilioni 3.9) na kampuni mbili za misitu, ili kuwawezesha wakulima kupanda miti kwa ajili ya biashara. Kampuni hizo ni New Forest Company(NFC) na Kilombelo Valley Teak Company(KVTC) ambapo makubaliano hayo ni ya miaka mitatu ya uendeshaji wa mradi huo utakaowezesha kupanda hekta 2000 za miti katika Maeneo ya Iringa,Njombe,Mbeya na Morogoro. Akizungumza leo(Alhamisi) Balozi wa Finland hapa nchini, Pekka Hukka amesema kiasi hicho cha fedha kitawezesha kuongeza kasi ya upandaji miti kwa wakulima wadogo wakati kampuni hizo zikiwa mteja wa miti hiyo. Soma zaidi…

Post a comment