HOTUBA YA MGENI RASMI MHE. PROF. JUMANNE A. MAGHEMBE (MB) WAZIRI WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII ILIYOSOMWA NA MKUU WA WILAYA YA MOROGORO MHE. REGINA CHONJO KWENYE SIKU YA KITAIFA YA UPANDAJI MITI TAREHE 1 APRILI, 2017 MKOANI MOROGORO

Ndugu Wananchi,
Tukumbuke kuwa MISITU YETU NI UHAI WETU na kwamba mahitaji mengi muhimu katika maisha yetu ya kila siku yanategemea misitu kwa njia moja au nyingine.  Napenda siku hii ya leo nizungumzie kuhusu Nishati itokanayo na miti. Sote tunajua kuwa, Nishati inayotokana na misitu ndiyo inayotegemewa na Watanzania takriban asilimia 90  kwa maisha yao ya kila siku.

Katika nchi yetu, kuna vyanzo mbalimbali vya nishati kwa matumizi ya wananchi, lakini nishati itokanayo na miti inafanya matumizi yanayofikia 85%, wakati nishati itokanayo na bidhaa za petroli ni 9.3%, Umeme ni 4.5% na makaa ya mawe na vyanzo vingine ni 1.2% tu ya mahitaji yote. SOMA ZAIDI CHINI
HOTUBA YA MGENI RASMI MHE – 1.4.2017
KUPANDA MITI KITAIFA 2017

 

 

Post a comment