Mgogoro wa Uongozi Mihima watishia Kuangamiza msitu wa Kijiji

Na. Ahmad Mmow, Lindi.

Mgogoro wa uongozi katika kijiji cha Mihima Wilaya ya Lindi, unatajwa kuwa unaweza kuangamiza msitu wa hifadhi wa kijiji hicho wenye ukubwa hekta 2662. Wakizungumza na Lindiyetu.co.tz mwanzoni mwa wiki hii kijijini hapo, baadhi ya wananchi na viongozi wa serikali ya kijiji hicho, walisema mgogoro huo ambao uliodumu kwa takribani miaka mawili, chanzo chake kikitajwa kuwa ni uamuzi wa wananchi kuuondoa uongozi wa kijiji hicho kutokana na tuhuma za ufisadi, umeathiri shuguli za maendeleo na kusabanisha uharibifu mkubwa wa msitu wa kijiji hicho.

Walisema tangu viongozi wa wilaya ya Lindi walipo urejesha madarakani uongozi huo ambao uliondolewa na wananchi hakuna shuguli zozote zinafanyika katika kijiji hicho na uongozi huo umesambaratika. Aliyekuwa kaimu mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho, Emillian Hokororo, alisema amejiuzulu nafasi hiyo ili kukwepa fedheha. Kwasababu hakuna mikutano mikuu ya kijiji na serikali ya kijiji inayofanyika. Kwasababu wajumbe wengi wamejiuzulu. Alisema halihiyo inasababisha kijiji hicho kukosa viongozi ndipo maliasili za kijiji ikiwamo msitu huo kuvunwa ovyo.

Mwananchi Issa Katenda alisema waliuondoa uongozi uliorejeshwa na mkuu wa wilaya ya Lindi baada ya kubaini ufisadi. Hata hivyo mkuu wa wilaya wawakati huo aliurejesha na kuuondoa uongozi wa muda uliokuwa umewekwa na wananchi hao. Ambapo aliamrisha yasifanyike matumizi yeyote ya fedha za kijiji hadi apelekwe mkaguzi akapitie hesabu zote za mapato na matumizi.“mkaguzi alikuja, lakini mpaka sasa hatuja letewa taarifa za ukaguzi huo, tangu wakati huo hadi sasa hakuna ushuru unaokusanywa. Aliyebaki ni mtendaji wa kijiji tu ambae nae anakaimu, hakuna vikao wala mikutano na msitu unaangamia,” alisema Katenda. SOMA ZAIDI

Post a comment