Mashaka Mgeta
SERIKALI ipo katika mchakato wa kuiboresha sera ya misitu ya mwaka 1998, hali itakayosaba- bisha marekebisho ya Sheria ya Misitu namba 12 ya mwaka 2012.
Afisa Misitu Mwandamizi ka- tika idara ya misitu na nyuki ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Emanuel Msofe, anasema hayo wakati akizungumza katika war- sha ya wahariri na waandishi wa habari waandamizi iliyoandali- wa na Jumuiko la Maliasili Tan- zania kupitia kampeni ya Mama Misitu.
Warsha hiyo iliyofanyika hivi wilayani Kibaha katika mkoa wa Pwani, ikahusisha pia ziara ya kuvitembelea baadhi ya vijiji miongoni mwa 11 vinavyozun- guka msitu wa Ruvu Kusini.
Msofe anasema kutokana na mabadiliko na changamoto kadha wa kadha zilizobainika katika kipindi cha tangu kupit- ishwa kwa sera hiyo hadi sasa (takribani miaka 19), imebainika kuwapo haja ya kufanya mabore- sho ya sera hiyo ili iweze kue- ndana na hali halisi kwa kadri ya mahitaji yaliyopo.
Kufanyika kwa maboresho ya sera hiyo kutaifa Serikali ifanye marekebisho ya Sheria ya Misitu yatakayojibu mahitaji ya kisera.
Kwa hali hiyo, ni wazi kwamba jitihada za kufanikisha mareke- bisho ya sera ya misitu ni zenye kuhitaji kuungwa mkono, kwa maana misitu ni miongoni mwa sekta zenye mchango mkubwa katika maisha ya kila siku ya watu, uchumi wa nchi na uhaki- ka wa hali nzuri ya hewa na maz- ingira ya kuishi viumbe hai.
Takwimu za Wakala wa Hudu- ma za Misitu (TFS) zinaonesha kuwa Tanzania ina jumla ya hek- ari milioni 48.1 ya misitu, ikiwa ni sawa na asilimia 55 ya ardhi ya nchi yenye kilomita za mraba945,087.
Hata hivyo, kutokana na mchakato wa maboresho hayo kuwa katika hatua za awali, hakuna taarifa zilizotolewa kuhusiana na uboreshwaji wa sera hiyo, ingawaje inahisiwa kwamba maeneo kama ushiriki wa umma katika usimamizi na uhifadhi wa misitu hasa inay- omilikiwa na Serikali Kuu.
Tofauti na inayomilikiwa na vijiji, misitu ya Serikali Kuu ili- yo chini ya TFS inakabiliwa na changamoto kubwa za ukosefu wa ulinzi, hali inayosababisha kuwapo kiwango kikubwa cha uharibifu na hujuma zinazo- fanywa na watu wasiokuwa na nia njema.
Umbali kutoka ofisi za TFS, upungufu wa wafanyakazi, vy- ombo vya usafiri na ufinyu wa bajeti ni miongoni mwa mambo yanayotajwa kwenye maeneo mengi yenye misitu ya Serikali kuwa yanachangia kufifisha jiti- hada za ulinzi wa rasilimali hiyo. Hata hivyo, mpango shirikishi wa umma (wakazi wa vijiji vina-vyoizunguka misitu hiyo) una- tumika kufanikisha ulinzi wa misiti ya Serikali Kuu, licha ya kuendelea kuwapo kwa changa- moto zinazoweza kuwa sehemu ya mahitaji katika sera ya misitu inayoboreshwa.SOMA ZAIDI