Ushiriki uwe nyenzo katika hifadhi ya msitu wa Ruvu Kusini

Na Mashaka Mgeta,

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Jumuiko la Maliasili Tanzania kupitia kampeni ya Mama Misitu, iliwakutanisha wahariri na waandishi waandamizi katika semina na ziara iliyowafikisha kwenye maeneo yenye msitu wa Ruvu Kusini mkoani Pwani.Ni mafunzo yaliyoibua hitaji la ‘nguvu zaidi’ katika kuchagiza kasi ya vyombo na waandishi wa habari kuelimisha, kutetea na kutoa taarifa zinazohusiana hifadhi ya misitu.

Takwimu zinazotokana na tath-mini ya rasilimali za misitu iliyofanyika mwaka 2013, zinaonesha kuwa tani mil-ioni moja za mkaa kila mwaka hutokana na ukataji wa misitu iliyopo kwenye eneo linalokadiriwa kuwa na ukubwa wa hekta milioni 48.1 nchi nzima.Pia utafiti uliofanywa na Wakala wa Hu-duma za Misitu (TFS) ulionesha kuwa ka-tika uhifadhi, Tanzania inapoteza hekta 400,000 za misitu kila mwaka kupitia matumizi ya kuni, mkaa, mbao, ujenzi na uchomaji moto misitu.Zipo athari nyingi zinazotokana na uharibifu wa misitu kiasi kwamba hata zikiorodheshwa na kufafanua hapa, nafasi iliyopo kwenye safu hii haitatosha.

Bonyeza hapa kusoma zaidi…

Post a comment