UTOROSHAJI MBAO NJE YA NCHI UNAVYOINYIMA TANZANIA MAPATO

UKUSANYAJI wa mapato kwa Serikali kutokana na mazao ya Misitu umepungua baada ya wafanyabiashara kujiusisha na utoroshaji wa mazao hayo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji wakikwepa kodi na tozo zinazotozwa nchini na mamlaka za serikali.

Afisa Forodha Mfawidhi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania mkoa wa mtwara (TRA) Sume Kunambi anasema athari za utoroshoji wa mazao ya misitu yakitokea madhara yake huwa ni makubwa kutokana na serikali inapoteza mapato kwa ajili ya kutoa huduma kwa jamii ambayo yangesaidia kununua dawa za hospital pamoja na ujenzi wa miundombinu.Uchunguzi wa makala haya umebaini kuwa wafanyabiashara wa mbao za miti aina ya Mkongo na Mninga wanalipa kodi ya sh. 235,520 kwa meta moja za ujazo wakati, wanaoingiza mbao kutoka Msumbiji wanalipa sh. 5,000 kupitia Mamlaka ya Mapato nchini (TRA). SOMA ZAIDI

Post a comment