WAHARIBIFU WA MAZINGIRA WAKAMATWE-MAJALIWA

Na. Ahmed Mmow, Ruangwa.
Waziri mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wananchi mkoani Lindi kutunza na kulinda misitu ili kuiepusha nchi kuwa jangwa.
Majaliwa ametoa onyo hilo leo kwa nyakati tofauti, alipozungumza na wananchi katika vijiji vya Nanjalu, Nambilanje, Mkalanga, Namichiga, Nandenje na Mandarawe vilivyopo katika wilaya ya Ruangwa.
Waziri Majaliwa ambae pia ni kiongozi wa shuguli za serikali bungeni, alisema uharibifu wa misitu licha ya kuharibu mazingira, lakini pia unasababisha serikali kutumia fedha nyingi katika kufanya tafiti na kuchimba visima vya maji kutokana na vyanzo vingi vya maji kukauka.
Alisema hali ya uharibifu wa misitu ikiendelea, kunauwezekano mkubwa wa nchi kugeuka jangwa. Hivyo kila mwananchi anawajibu wakuilinda na kuitunza. SOMA ZAIDI

Post a comment